Zaidi ya wagonjwa 300 wa mifupa wamepatiwa huduma kwa siku moja katika kambi maalum ya matibabu ya mifupa, inayotolewa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Akizungumza na wananchi waliokusanyika hospitalini hapo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, amewahimiza wakazi wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kapata huduma hiyo kwani imepunguza gharama ya matibabu Kwa kusafiri umbali mrefu hadi jijini Dar es Salam
Rc Malima ametoka wito huo alipokuwa akitembelea kambi ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia kutoka Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI). Alisema kambi hiyo ilipanga kuhudumia wagonjwa 500 kwa siku nne, lakini tayari zaidi ya wagonjwa 300 wamejiandikisha kwa siku moja pekee ili kufanyiwa vipimo na kupata ushauri wa kitaalamu
“… hadi sasa, wagonjwa zaidi ya 300 wameshapatiwa matibabu, hivyo wananchi mnapaswa kujitokeza kwa wingi ili kupata matibabu kutoka kwa madaktari hawa bingwa
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili, Dkt. Lemeri Mchome, aliwataka wananchi kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kama vile shinikizo la damu. Alisisitiza pia umuhimu wa kutoa muda wa kupumzika ili kuimarisha kinga ya mwili.
Vilevile, Dkt. Mchome alihimiza wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo ya mifupa, nyonga, miguu, na magonjwa mengine kufika kambini hapo kwa ajili ya matibabu.