Mwanadiplomasia mkuu wa Iran amemuonya mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwamba Tehran iko tayari kwa jibu la “maamuzi yoyote ya kujutia” ikiwa Israel itaishambulia nchi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi alisema, “Iran, wakati ikifanya juhudi za kila namna kulinda amani na usalama wa eneo hili, iko tayari kikamilifu kwa jibu la uhakika na la majuto kwa matukio yoyote yanayotokea.”
Mnamo Oktoba 1, Iran ilirusha karibu makombora 200 katika Israeli, shambulio lake la pili la moja kwa moja kwa nchi hiyo katika kipindi cha chini ya miezi sita.
Mengi ya makombora hayo yalinaswa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel, huku mengine yakipiga kambi za kijeshi, lakini hakuna uharibifu mkubwa au hasara iliyoripotiwa.
Iran ilisema kuwa makombora hayo yalirushwa ili kulipiza kisasi mauaji ya mkuu wa Hezbollah Hassan Nasrallah ambaye aliuawa na mashambulizi ya anga ya Israel katika mji mkuu wa Lebanon Septemba 27.