Kocha mkuu mpya wa England Thomas Tuchel anasema anaelewa utata kuhusu uteuzi wake lakini anatumai rekodi yake kwenye Premier League akiwa na Chelsea inampa “makali ya Uingereza kwenye pasi yake ya Ujerumani”.
Tuchel, ambaye ametia saini kandarasi ya miezi 18 na kibarua cha kushinda Kombe la Dunia la 2026, ni kocha wa tatu wa kigeni katika historia ya England baada ya Mswidi Sven Goran-Eriksson na Muitaliano Fabio Capello.
Mark Bullingham, mtendaji mkuu wa FA, alifichua bodi inayoongoza iliyohojiwa “takriban wagombea 10” kufuatia kujiuzulu kwa Gareth Southgate mwezi Julai, baadhi yao wakiwa Waingereza, lakini akasisitiza “wanawiwa na mtu anayeweA kiwapatia nafasi nzuri ya kushinda kombe” kwa kumteua Tuchel.
Kocha huyo wa zamani wa Bayern Munich anatumai kuwa miezi 18 aliyokaa Chelsea, ambayo aliiongoza hadi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa 2021, itawashawishi wafuasi wake “shauku” na “heshima” yake kwa Uingereza, licha ya uraia wake
“Nasikitika kuwa na pasipoti ya Ujerumani lakini ninaweza kuwaambia tu … na labda wafuasi wanaweza kuhisi mapenzi yangu kwa Ligi Kuu ya Uingereza, mapenzi yangu kwa nchi, jinsi ninavyopenda kuishi na kufanya kazi hapa,” Tuchel, 51, Alisema katika utambulisho wake Wembley siku ya Jumatano