Jamhuri ya Congo imesitisha safari za mawaziri na maofisa nchini humo hadi mwishoni mwa mwaka, serikali ya nchi hiyo imesema siku ya Jumatano.
“Safari zote za nje za mawaziri na maofisa wengine wa serikali zenye kutumia fedha za umma zimesitishwa mpaka mwisho wa mwaka 2024,” ilisema taarifa ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Anatole Collinet Makosso.
“Ruhusa maalumu itatolewa tu kwa safari zinazomhusu Rais wa Jamhuri,” ilisema nakala ya taarifa hiyo kama ilivyonukuliwa na AFP.
“Hatua hiyo inalenga kupunguza gharama za serikali, ambayo inakabiliwa na changamoto kubwa ya kifedha “, chanzo cha serikali kiliiambia AFP.
“Sehemu kubwa ya uchumi wa Congo imekuwa ikipitia changamoto kubwa ya kifedha,” kilisema chanzo hicho.