Jamii imetakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya vipodozi yanayoendana na asili ya ngozi zao ili kuepusha madhara ya kiafya yanayoeeza kujitokeza kutokana na kutumia vipodozi vyenye viambata vya sumu
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na daktari bingwa wa ngozi kutoka hospitali ya taifa ya muhimbili Dkt. Andrew Foi wakati wa uzinduzi wa bidhaa za ngozi zilizotengenezwa na kampuni ya Betty World ambapo pia ameiomba serikali kuendelea kuwekeza katika kuwezesha upatikanaji wa wataalamu wa ngozi ili kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na matumizi sahihi ya bidhaa za ngozi
Kwa upande wake Dkt Elizabeth Consoli ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Betty world ameeleza kuwa bidhaa hizo zimezingatia utengenezaji wa bidhaa za ngozi zinazoendana na uhalisia wa ngozi ili kuepusha madhara huku akibainiaha kuwa tafiti nyingi zilizofanywa katika kutengeneza bidhaa za vipodozi hazikuhusisha uhalisia wa ngozi za kiafrika
Naye mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo Meshack Lutembeka ameeleza kuwa lengo ni kuanzisha kampuni za kizawa zitakazosaidia kulinda afya za watanzania lakini vilevile kuongeza mapato ya fedha za kigeni yanayotokana na kuuza bidhaa zinazozalishwa nchini katika masoko kimataifa.