Erik ten Hag amesisitiza kuwa hakujawa na mazungumzo ya ndani kuhusu hatma yake kama meneja licha ya mwanzo mbaya wa Manchester United msimu huu.
Ten Hag yuko kwenye presha akiwa na United katika nafasi ya 14 kwenye jedwali la Premier League baada ya kushinda mara mbili pekee kati ya mechi saba.
Mkutano wa bodi uliofanyika wakati wa mapumziko ya kimataifa, ukiongozwa na mmiliki mwenza Sir Jim Ratcliffe, haukutoa taarifa zaidi kuhusu msimamo wa Mholanzi huyo
“Kelele pekee ni kutoka kwa vyombo vya habari,” Ten Hag aliambia mkutano wa wanahabari siku ya Ijumaa. “Baadhi yenu [vyombo vya habari], sio nyote, mnaleta hadithi, kuunda hadithi, kutengeneza hadithi, kuleta uongo kwa sababu sote tuko kwenye ukurasa mmoja klabu hii.
“Nilisema kabla ya mapumziko — waandishi wa habari kadhaa [walisema] hawakuniamini na naona ripoti hizo — ndani ya klabu ni kimya.”