Hamas imebainisha hivi punde siku ya Ijumaa, Oktoba 18, kwamba mateka wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza hawataachiliwa hadi Israel itakapokomesha mashambulizi yake.
Kauli hii inajiri saa chache baada ya kundihili la Palestina kuthibitisha kifo cha kiongozi wake Yahya Sinwar.
Kifo chake kimeibua matumaini ya uwezekano wa kumalizika kwa mzozo huo, ambao tayari umeua zaidi ya Wapalestina 40,000, 80% yao wakiwa wanawake na watoto, kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza
Hamas ilithibitisha siku ya Ijumaa Oktoba 18 kifo cha kiongozi wake Yahya Sinwar katika matangazo ya video yaliyorushwa kwenye kituo cha Al Jazeera, na kukataa kuwaachilia mateka wa Israel wakati “uchokozi” wa Israel dhidi ya kundi hilo ukiendelea kutoka Gaza.
Kifo chake hata hivyo kilikuwa kimetia matumaini, hasa miongoni mwa nchi za Magharibi, ya uwezekano wa kumalizika kwa mzozo huo. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amebainisa kwamba kifo hiki kilikuwa alama ya “mwanzo wa mwisho” wa vita huko Gaza.