Korea Kaskazini ilidai Jumamosi kuwa iligundua mabaki ya angalau ndege moja ya kijeshi ya Korea Kusini iliyoanguka katika mji mkuu Pyongyang, ikitoa picha za kifaa ambacho baadhi ya wachambuzi walithibitisha kuwa ni cha Korea Kusini.
Kaskazini yenye silaha za nyuklia hivi majuzi iliishutumu Seoul kwa kutumia ndege zisizo na rubani kudondosha vipeperushi vya propaganda dhidi ya serikali kwenye mji mkuu.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Pyongyang alisema mamlaka za usalama zilipata mabaki ya ndege isiyo na rubani iliyoanguka wakati wa msako katika mji mkuu wa Korea Kaskazini mnamo Oktoba 13, shirika rasmi la habari la KCNA liliripoti.
Uchunguzi wa Korea Kaskazini “ulithibitisha kisayansi kwamba ndege hiyo isiyo na rubani ilitoka kwa ROK,” msemaji huyo ambaye hakutajwa jina, akitumia kifupi cha Korea Kusini.
Awali wanajeshi wa Korea Kusini walikanusha kutuma ndege zisizo na rubani lakini wamekataa kutoa maoni yao.
“Hakuna thamani katika kuthibitisha au kujibu madai ya upande mmoja ya Korea Kaskazini,” ilisema katika taarifa fupi Jumamosi.
Korea Kaskazini hapo awali ilionya kuwa ingechukulia kama “tangazo la vita” ikiwa ndege nyingine isiyo na rubani itagunduliwa.