Kampeni ya Tuwaambie Kabla hawajaharibiwa Ilivyopokelewa Ngara Sekondari,waombwa kupaza sauti vitendo vya ukatili.
Kampeni ya Jeshi la Polisi tuwaambie kabla hawajaharibiwa imeendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali ya Shule za awali, Msingi na Sekondari pamoja na vyuo wilayani Ngara Mkoa wa Kagera..
Akitoa Elimu hiyo katika Shule ya Sekondari Ngara Mkuu wa dawati la Jinsia na watoto Wilayani humo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Hadija Mfinanga amesema kampeni hiyo imelenga wanafunzi ambao wapo katika changamoto ya ukatili ambapo kupitia kampeni hiyo inakwenda kuwajenga kifikra na kuwafanya wajiamini katika kupaza sauti juu ya vitendo vya ukatili.
Mkaguzi Mfinanga amewataka wazazi, walezi pamoja na walimu kuongea na wanafunzi hao juu ya madhara ya ukatili huku akisisitiza kuwa ukatili unamuathiri mwanafunzi kimasomo akiwaomba kuwa karibu na kuwaambia juu ya vitendo hivyo ili wapate maendeleo mazuri kitaaluma.
Aidha amewataka wanafunzi kutambua kuwa wao pamoja na Jamii wanayoishi nayo inaimani kubwa na wao katika maendeleo ya kielimu akiwataka kutokukubali kurubuniwa na mtu ama kundi la watu ambao wana malengo mabaya katika maendeleo yao kitaaluma.
Vilevile amewaomba kutoa taarifa kwa wazazi wao pamoja na walezi endapo watafanyiwa vitendo vya ukatili huku akiwasihi pia kuwatumia viongozi wa dini na Jeshi la Polisi pale inapodi endapo wanafanyiwa vitendo vya ukatili.