Imeripotiwa kuwa Beyoncé amemuunga mkono na taonekana kwenye kampeni ya Kamala Harris huko Houston siku ya Ijumaa, kulingana na gazeti la Washington Post,wakati makamu wa rais atakapozuru mji alikozaliwa mwanamuziki huyo wa pop kuandamana na mgombea wa Seneti ya Kidemokrasia Colin Allred na kushambulia marufuku ya utoaji mimba iliyopitishwa na Republican.
Wimbo wa Beyoncé “Freedom” huchezwa mara kwa mara katika hafla za kampeni za Harris, ingawa mwimbaji huyo hajaonekana na makamu wa rais tangu alipoanzisha kampeni yake.
Harris amekuwa akipokea ridhaa za wanamuziki kadhaa mashuhuri katika wiki za hivi karibuni, akiwemo Taylor Swift na Bruce Springsteen, ambao watafanya matamasha na kampeni inayoanza leo huko Atlanta