Chama cha ngumi Morogoro kwa kushirikiana na wadau wengine wameanza mpango juibua vipaji vya Mchezo huo Kwa watoto wa kike Ili kuleta hamasa ya Kushiriki na ajira kwa vijana.
Debora Mwenda ni mmoja wa bondia wanawake Mkoani Morogoro anasena tangu ameanza kushiriki mchezo huo amekua anajitenga na makundi mbalimbali ya mtaani ikiwemo vitendo viovu.
Anasema awali aliogopa kuingiza katika mchezo huo kwa sababu ya baadhi ya watu kuona Kama Mchezo wa kihuni na wanawake hawapaswi kucheza jambo ambalo halina ukweli wowote .
Anasema tangu aanze kucheza mchezo huo ni miaka mitatu imepita saaa licha ya kutofanya vizuri lakini malengo yake kuwa mchezaji mkubwa wa kulipwa mchini.
Naye Charles Mbwana maarufu ambaye ni mwalimu wa bondia wa ngumi za kulipwa Nchini Twaha Kiduku amesema mpango uliopo kuhakikisha anaibua vipaji Kwa mabondia wachanga ikiwemo na wanawake.
Naye mdau wa Mchezo wa Ngumi Bakari Khatibu kutoka Peak Time anasema katika kuhakikisha mchezo unaleta manufaa hasa kwa vijana Kwa kuwapa nafasi ya kucheza mara Kwa mara
“Kesho katika ukumbi Tanzanite hapa Morogoro Kuna pambano kubwa lakini tulichofanya tumechukua mabondia kutoka Morogoro na Dar es Salam na wengi wao ni mabondia vijana ”
Juma Mbena ni mkazi wa Morogoro anasema mchezo wa ngumi Kwa Sasa umeleta ajira kubwa kwa vijana Kwa jinsia zote kike na kiume hivyo wazazi waache kukatisha tama watoto wao hasa wakike pindi wanapotaka kuingia katika mchezo huo.
Naye bondia mkongwe kutoka Morogoro Cosmas Cheka ambaye mwekazina chama cha ngumi Morogoro amesema wanaendela kutoa elimu kwa wazazi ili kuruhusu watoto kuingia katika mchezo huo.
Amesema zamani mchezo huo ulikua hauna faida lakini kwa Sasa umekua na faida na manufaa makubwa ambapo mabondia wachanga nao wameanza kujiunga katika vyama hivyo.
Anasema licha ya kupata manufaa kwa bondia kulata uligoni mara kwa mara lakini pia mabondia watapa elimu ya ujasirimali,kujitambua na masuala ya kujilinda na matumizi ya dawa za kulevya.