MAADHIMISHO ya Siku ya Shampeni 2024 yaliyoandaliwa na kinywaji maarufu cha Moët & Chandon yamkutanisha Mwanzilishi wa Kampuni Kubwa ya Ushonaji ya Bespoke Clothing, Mtani Nyamakababi na watu wenye vipaji mbalimbali wenye vipaji Afrika ili kubadilishana uzoefu wa kazi zao
Tukio hilo liliandaliwa katika eneo maarufu linalojulikana kama Épernay nchini Ufaransa, huku likilenga kusherehekea mafanikio ya miaka mingi ya Moët & Chandon katika tasnia ya sanaa, na ubunifu na kutokea fursa kwa wabunifu wa Kiafrika kukutana na kubadilishana uzoefu wa kazi zao.
Tukio hilo lilihusisha wabunifu maarufu saba kutoka Afrika Mtani Nyamakababi akiwa ni mmoja wao kutoka Tanzania akiwa ni mwanzilishi wa kampuni tajwa hapo juu.
Wengine walihusisha vipaji vya mavazi, muziki, na upigaji picha, wakiwemo Thebe Magugu kutoka Afrika Kusini, Banke Kuku kutoka Nigeria, Aisha Ayensu kutoka Ghana, Mahine Sef kutoka Cameroon, Lyra Aoko kutoka Kenya, na Youssra Nichane kutoka Morocco.
Nyamakababi amesema ziara hiyo ilikuwa ni ya kuvutia hasa alipopata nafasi ya kutembelea Moët & Chandon na kuona wanavyotilia mkazao juu ya ubora na umakini katika utengenezaji wa kila chupa ya shampeni.
Ameongeza kuwa uzoefu huo umetengeneza historia nzuri katika safari yake yake na utendaji kazi wake na kuwa alichoona alipotembelea Moët & Chandon ilimfanya afikirie namna ya kuboresha uwezo wake katika ubunifu wa mavazi.