Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alikataa mpango uliopendekezwa na Misri jana wa kusitisha mapigano kwa muda mfupi na Hamas katika Ukanda wa Gaza, Shirika la Anadolu liliripoti.
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi alitangaza pendekezo hilo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel.
“Tulipendekeza kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza kwa siku mbili ili kubadilishana mateka wanne (Waisraeli) kwa baadhi ya wafungwa (wa Palestina), na kisha mazungumzo yatafanyika kwa siku 10 ili kugeuza usitishaji mapigano kuwa mapatano ya kudumu…