Utendaji mbovu wa biashara kwa nchi za bara la Afrika pamoja na uwezo mdogo wa kujadili makubakiano ya kibiashara ya kikanda na kimataifa kumetajwa kama miongoni mwa changamoto zinazokwamisha ufanisi wa nchi za ukanda wa Afrika masharikikwenye soko la kimataifa.
Hayo yameelezwa na Naibu katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Balozi Dkt. John Simbachawe wakati akizindua Warsha ya 28 ya Taasisi ya REPOA ya kuchakata Taarifa kuhusu ukuaji wa biashara na soko lenye ushindani kwa nchi za Africa mashariki.
Dkt. Simbachawene Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo nchi za afrika zinawajibu kujikita katika kusimamia mikakati wanayojiwekea. Ikiwa ni pamoja na kutathimini matokeo ya juhudi za wadau husika kwenye sekta hiyo.
Tafiti na Uzoefu wa Taasisi ya REPOA unabainisha utofauti ushindaji na ufanisi wa kibiashara baina ya nchi za Africa Mashariki na Mataifa mengine hususani katika suala la ubora na viwango vya bidhaa zinazoingia kwenye solo la ushindani.