Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.Albert Chalamila anatarajiwa kuongoza mkutano mkuu wa Tano wa Bodi ya usajili wabunifu majengo na wakadiriaji ujenzi, siku ya tarehe 29 oktoba mwaka 2024 katika kumbi ya mikutano ya kimataifa ya Mwalimu Julius Nyerere .
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Bodi ya usajili wabunifu majengo na wakadiriaji ujenzi dkt. Ludigija Bulamile , amesema mkuu wa mkoa ataongoza mkutano huo wa tano ambao unawakutanisha wataalamu katika sekta ya ujenzi kuweza kujadili na kuangalia fursa mbalimbali zilizopo kwenye sekta hiyo kupitia teknolojia mpya na zakisasa.
Dkt.Ludigija akizungumza mapema hii leo katika ofisi za bodi ya usajili amewataka wadau wote katika sekta ya ujenzi kuweza Kufika katika mkutano huo wa tano ili kuweza lujadili kwa pamoja namna ya kuweza kushindana na taasisi za kimataifa.
“Kesho ni siku muhimu sana kwetu sisi wasanifu majengo , mkuu wa mkoa wa Dar es saalam ndugu Albert Chalamila ataongoza mkutano wetu kama Mgeni rasmi akimuwakilisha naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Mhe.Dotto Biteko, wahandisi na wasanifu majengo turaonesha kazi zetu kupitia teknolojia ya kisasa huku tukijadili fursa mpya kwenye tasnia hii”.
Aidha kwa upande wake Msajili wa bodi ya wabunifu majengo na wasanifu majenzi Arch.Edwin Nnunduma amesema bodi hiyo kupitia wadau wengine wamejipanga kuonesha kazi zao mbalimbali zinazofanywa katika miradi ya kimaendeleo na ya kimkakati, huku akiwasisitiza wananchi kuweza kutumia wataalamu wa ndani kwenye ujenzi wa nyumba na majengo mengine ilikupunguza gharama.
“Unaweza ukatumia gharama ndogo sana kama utatumia wataalamu kukupatia ushauri kwa sasa teknolojia imekuwa Msaada kwetu hivyo tunafanya kazi kwa weledi mkubwa na gharama nafuu huku tukikuhakikishia usalama wa jengo lako na ubora uliokizi viwango”.
Mkutano wa wabunifu majengo na wasanifu majenzi utafanyika kwa siku mbili siku ya tarehe 29 na 30 oktoba huku Mhe.Albert Chalamila akiwa ndio mgeni rasmi katika mkutano huo .