Vinicius Jr alitumia mitandao ya kijamii baada ya kushika nafasi ya pili katika kura ya tuzo za Ballon d’Or nyuma ya Rodri wa Manchester City baada ya Real Madrid kuongoza kususia sherehe za Jumatatu usiku kupinga matokeo hayo.
Vinicius alikuwa anapendekezwa na wengi kushinda tuzo ya wanaume baada ya msimu uliomalizika, lakini wajumbe wa Real Madrid walighairi safari yao ya sherehe ya Paris dakika za mwisho baada ya matokeo kuvuja ya tuzo hiyo ya kifahari yalionyesha Rodri alipata kura nyingi zaidi kabla ya Mbrazil na Jude Bellingham.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye alitawazwa mchezaji bora wa mwaka wa Ligi ya Mabingwa baada ya kucheza nafasi ya nyota katika Kombe la 15 la Uropa la Real Madrid, alitumia Twitter/X na kutuma
aliandika “I’ll do it 10 times if I have to. They’re not ready.”
”Nitafanya hivyo mara 10 ikibidi. Hawako tayari.”