Cristiano Ronaldo anamtaka mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba kuchezea Al Nassr ya Saudi Arabia atakaporejea kutoka kwa marufuku yake ya kutumia dawa za kusisimua misuli, inasema TuttoJuve.
Pogba, 31, awali alipigwa marufuku ya miaka minne kwa matumizi ya dawa za kusisimua misuli lakini akapunguza marufuku yake hadi miezi 18 na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) baada ya kukata rufaa mapema mwezi huu, kumaanisha kwamba anaweza kurejea katika soka ya kulipwa Machi 2025.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alifichulia ESPN kwamba alifikiria kustaafu, akikiri kwamba inabidi awe “angalifu zaidi” baada ya kuchukua kirutubisho ambacho kilikuwa na dutu iliyopigwa marufuku.
Lakini kiungo huyo anaporejea uwanjani, huenda akahamia kwa miamba ya Saudi Pro League, Al Nassr, huku Ronaldo mwenye umri wa miaka 39 akiwa na nia ya kusaidia kumsajili mchezaji mwenzake wa zamani.