Mamlaka ya Guinea ilifuta makumi ya vyama vya siasa na kuweka viwili vikuu vya upinzani chini ya uangalizi mwishoni mwa Jumatatu, wakati serikali ya mpito bado haijatangaza tarehe ya uchaguzi.
Nchi hiyo ya Afrika Magharibi imekuwa ikiongozwa na utawala wa kijeshi tangu wanajeshi walipomwondoa madarakani Rais Alpha Conde mwaka 2021.
Jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi inayojulikana kwa jina la ECOWAS imeshinikiza kurejeshwa kwa utawala wa kiraia na uchaguzi umepangwa kufanyika 2025.
Kuvunjwa kwa wingi kwa vyama 53 vya siasa na kuwekwa kwa vyama vingine 54 chini ya uangalizi wa miezi mitatu ni jambo halijawahi kutokea nchini Guinea, ambayo ilifanya uchaguzi wake wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 2010 baada ya miongo kadhaa ya utawala wa kimabavu.
Wizara ya Utawala wa Wilaya na Ugatuaji ilitangaza hatua hizo kulingana na tathmini ya vyama vyote vya kisiasa iliyoanza Juni. Tathmini hiyo ilikusudiwa “kusafisha ubao wa chess wa kisiasa,” kulingana na wizara