Waigizaji wa Avengers wameonyesha kuunga mkono kampeni ya Kamala Harris siku chache kabla ya Uchaguzi wa Urais wa 2024 wa Marekani .
Katika video iliyotolewa na Vanity Fair mnamo Oktoba 31, waigizaji Robert Downey Jr., Chris Evans, Scarlett Johansson, Mark Ruffalo, Don Cheadle, Danai Gurira, na Paul Bettany waliigiza tena uhusika wao maarufu wa Marvel ili kuwahimiza wapiga kura kumuunga mkono Harris.
Video ya sekunde 90 inaanza na Johansson akiwaita waigizaji wenzake, ambapo wanajadiliana mawazo kwa kauli mbiu ya Harris “Down with Democracy,” ambayo wanageuza kuwa picha za mtindo wa Marvel kwa kuisaidia kampeni ya Harris/Walz kisha video inahitimishwa kwa kuwakmbusha watazamaji kupiga kura tarehe 5 Novemba.