Mgombea urais wa Marekani Donald Trump amewasilisha kesi mahakamani dhidi ya kituo cha televisheni cha Marekani kwa kile anachoita mahojiano ya “kupotosha” na mpinzani wake Kamala Harris.
Kesi dhidi ya CBS News iliyowasilishwa katika mahakama ya Texas siku ya Alhamisi ilidai mtandao huo ulipeperusha majibu mawili tofauti kutoka kwa mgombea urais wa chama cha Democratic Kamala Harris alipokuwa akijibu swali kuhusu vita kati ya Israel na Hamas huko Gaza.
Toleo ambalo lilipeperushwa wakati wa kipindi cha Dakika 60 mnamo Oktoba 6 halikujumuisha kile kesi ilichoita jibu la “saladi ya neno” kutoka kwa Harris kuhusu ushawishi wa utawala wa Biden juu ya mwenendo wa vita wa Israeli.
Kesi iliyowasilishwa na mgombea mteule wa urais wa Chama cha Republican kimsingi ilishutumu CBS kwa kuhariri majibu ya Harris ili kuifanya ionekane wazi zaidi.
Kesi hiyo imewasilishwa katika mahakama ya shirikisho katika jiji la Texas la Amarillo, ambalo lina hakimu mmoja tu – Matthew Kacsmaryk.
Ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zilisema mahakama ya jaji aliyeteuliwa na Trump imekuwa chaguo maarufu kwa kesi zilizowasilishwa na Republican.