Safari ya kwanza ya treni ya kisasa ya Electric Multiple Unit (EMU) maarufu kwa jina treni ya Mchongoko imeanza rasmi leo November 1, 2024 kutoka Stesheni Magufuli DSM hadi Stesheni Kuu ya Samia mkoani Dodoma.
Treni Mchongoko ina vichwa mbele na nyuma tofauti na treni za awali zenye kichwa kimoja pia imeundwa kwa vipande nane ambavyo havitenganishiki tofauti na zile za kawaida ambazo unaweza kupunguza vipande
Inabeba jumla ya abiria 589, inatembea kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa 1.
Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amesema kuwa treni hiyo ya ‘express’ haitasimama njiani kama nyingine lengo likiwa ni kurahisisha safari kwa wasafiri wenye haraka kwani inapunguza muda wa kusafiri njiani kwa dakika 45.
Pia amesema kuanza kwa huduma za treni ya mchongoko ni kuongeza idadi ya kusafirisha abiria kwakuwa hivi sasa kutoka DSM hadi Dodoma wanasafirisha abiria zaidi ya elfu 9 hadi elfu 10 kwa siku.