Mwanamke wa Marekani ambaye anadai alitekwa nyara na viumbe wageni ‘Aliens’ ameishtaki Netflix, akisema kuwa filamu ya “The Manhattan Alien Abduction” inamuonyesha yeye kama mhalifu .
Linda Napolitano, ambaye sasa ana umri wa miaka 77, aligonga vichwa vya habari kwa mara ya kwanza mwaka wa 1989 alipodai kwamba alichukuliwa na Aliens kutoka kwenye nyumba yake ya ghorofa ya 12 huko Lower Manhattan.
Katika madai yake, Napolitano alisema, “Walinichukua hadi juu. [Sehemu ya anga ya juu]ilifunguka kwa utulivu kisha mimi nikajikuta ndani. Nikafunga macho yangu. sikutaka kuona.” Alielezea kuchunguzwa na viumbe wa kigeni na alijihisi kama panya wa maabara.
Hadithi yake inasemekana ilifafanuliwa baadaye katika kitabu cha mtafiti wa UFO Budd Hopkins.
Miaka mingi baadaye, alidai kwamba viumbe hao walilenga familia yake, na kuwafanya wateseke kutokana na “kutokwa damu puani.”
Mwanawe, Johnny, ambaye alionekana kwenye filamu na utambulisho wake ukiwa umefichwa, alisema, “Lazima liwe jambo la kutisha na lisilo na matumaini ambalo nimewahi kuhisi na ninaogopa.”
Mwanamke huyo anaamini kuwa hati hizo za Netflix zilizo muonesha yeye kama mtu aliyefurahishwa na kitendo hicho cha kuchukuliwa bila idhini yake na viumbe hao aliodai walimchukulia kama kitu cha kuchunguzwa maabara zitaharibu sifa yake kama “mtu mwaminifu na mzuri.”