Takriban watu 10 wameuawa baada ya mlima wa volcano kulipuka nchini Indonesia na kusababisha majivu mazito juu angani na kunyesha kwenye nyumba zilizo karibu.
Mlipuko huo katika Mlima Lewotobi Laki Laki, katika kisiwa cha Flores, baada ya saa sita usiku siku ya Jumatatu, ulimwaga majivu ya hudhurungi yenye urefu wa mita 2,000 (futi 6,500) angani.
Nyumba kadhaa ziliteketea kwa moto, ikiwa ni pamoja na nyumba ya watawa wa Kikatoliki, afisa wa eneo hilo Firman Yosef alisema.
Waokoaji wanatafuta miili zaidi chini ya nyumba zilizoporomoka.
Waliouawa hadi sasa, akiwemo mtoto, walipatikana na eneo la maili 2.4 la kreta.
Takriban watu 10,000 wameathiriwa na mlipuko huo katika vijiji sita vya wilaya ya Wulanggitang na vinne katika wilaya ya Ile Bura.
Serikali ya mtaa inajiandaa kutumia shule kama makazi ya muda kwa wale walioathirika.