Meneja wa muda wa Manchester United Ruud van Nistelrooy anasema hana mawasiliano na kocha anayekuja Ruben Amorim tangu ilipofichuliwa kuwa atakuwa mrithi wa Erik ten Hag Old Trafford.
Van Nistelrooy alikuwa msaidizi chini ya Ten Hag na haijafahamika iwapo atasalia kuwa sehemu ya wakufunzi katika klabu hiyo au kama Amorim atawasili na timu yake.
Baada ya United kutoka sare ya 1-1 na Chelsea kwenye Premier League, Van Nistelrooy alisema: “Sijazungumza naye [Amorim] na kwa sasa hakuna chochote kilichopangwa kwa mazungumzo yoyote.
“Ninafanya kazi yangu kwa sasa kuandaa Alhamisi [v PAOK katika UEFA Europa League] na mchezo wa Jumapili [v Leicester kwenye Ligi ya Premia] na kwa sasa nasubiri [kuona] jinsi mambo yanavyoendelea mawasiliano kuelekea kocha mkuu mpya.
“Imekuwa ngumu sana kutoka Jumatatu iliyopita hadi leo. Siku sita Ni wazi, inasikitisha sana kuona Erik akiondoka.”
Amorim atachukua rasmi mikoba ya United mnamo Novemba 11 – mara tu atakapokuwa ametimiza wajibu wake na Sporting Lisbon.