Xabi Alonso anarejea Anfield kwa mara ya kwanza Novemba 5, wakati timu yake ya Bayer Leverkusen ikimenyana na Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa, kombe ambalo aliwasaidia Wekundu hao kushinda 2005.
Aliichezea Liverpool mechi 210 kati ya 2004 na 2009, huku jambo kuu bila shaka likiwa kurejea kwa muujiza katika ushindi wao wa fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya AC Milan mjini Istanbul, Uturuki.
Mhispania huyo aliifungia Liverpool bao la tatu ndani ya dakika saba na kuwafanya wawe 3-3 kabla ya kwenda kushinda kwa mikwaju ya penalti.
Alonso, 42, anasalia kupendwa sana na mashabiki wa Liverpool na angeweza kuwa kwenye dimba la nyumbani kama mambo yangeenda tofauti.
Msimu uliopita, baada ya uamuzi wa kushangaza wa Jurgen Klopp kuondoka klabuni hapo, mashabiki wa Liverpool – ambao walikuwa wametambua mwendo wa ajabu wa Alonso huko Leverkusen – walikuwa na matumaini kwamba anaweza kuelekea Merseyside.