Serikali kupitia Mamlaka ya udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) imesema itaendelea kuweka mazingira mazuri katika matumizi ya Teknolojia na Tehama kwa lengo la kurahisisha Ununuzi wa umma na kuweka usimamizi.
Hayo yamebainishwa leo na Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) Dennis Simba katika Mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambapo amesema Serikali imetengeneza mazingira mazuri na wezeshi ambapo ndani ya Afrika Mashariki mfumo wetu ndo unafanya vizuri kuliko mifumo yote.
“Serikali ya awamu ya sita kupitia Mamlaka ya udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) tumefanikiwa kuokoa zaidi ya Billioni 15 kupitia ukaguzi, PPRA tunachofanya ni kukagua Miradi na zabuni zinapotolewa kwani ni jukumu letu na inasaidia kuokoa fedha nyingi katika miradi mbalimbali” Amesema Simba.