Baada ya Trump wa chama cha Republican, Jumatano kushinda kinyang’anyiro cha urais baada ya Fox News kukadiria kwamba alikuwa amemshinda Kamala Harris wa Democratic, jambo ambalo limerejesha ushawishi wake kisiasa miaka minne baada ya kuondoka Ikulu ya White House.
“Marekani imetupa mamlaka ambayo haijawahi kufanyaka na yenye nguvu,” alisema mapema Jumatano akihutubia umati wa wafuasi wake katika Kituo cha Mikutano cha Kaunti, Palm Beach.
Vyombo vingine vya habari havikuwa vimetangaza mshindi wa kinyang’anyiro cha urais, lakini alionekana kukaribia kushinda baada ya kuwa kifua mbele katika majimbo yenye ushindani ya Pennsylvania, North Carolina na Georgia na kuongoza katika mengine manne, kulingana na Edison Research.
Donald Trump amepata ushindi wake wa kwanza mkubwa katika kinyang’anyiro cha kuwania Ikulu ya White House kwa kushinda jimbo muhimu la North Carolina, ambalo alikuwa ameshinda mwaka 2016 na 2020 lakini ambalo lilitamaniwa sana na mpinzani wake Kamala Harris, kulingana na vyombo vya habari vya NBC, ABC na CNN.
Kinyang’anyiro cha kuingia katika Ikulu ya White House kati ya mgombea wa chama cha Republican Donald Trump na mgombea wa chama cha Democratic Kamala Harris kinaonekana kuwa kikali, huku taifa hilo likisubiri kwa hamu matokeo ya mojawapo ya uchaguzi mkali zaidikatika historia ya Marekani
Matokeo ya uchaguzi huo yataamua iwapo yatamuweka madarakani Harris na kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya kuliongoza taifa hilo lenye nguvu duniani, au kumrejesha Trump madarakani.