Katika hali ya kushangaza katika Bunge la Uganda hii leo wabunge waliingia katika Mjadala mkali ulisababisha ugomvi na mapigano na kupelekea kuahirishwa kwa shughuli za bunge.
Tukio hilo lilitokea wakati wa kikao cha mashauriano kilichohusu Mswada wa Kitaifa wa Marekebisho ya Kahawa ya 2024 ambapo mgogoro huo uliongezeka haraka, na kusababisha Mbunge Zaake kushambuliwa na baadaye kusafirishwa hadi hospitali kwa matibabu.
Mvutano ulianza kuibuka pale Zaake alipoeleza wasiwasi wake kuhusu usalama ndani ya Bunge, akidai kuwa watu ambao si Wabunge waliingia ndani ya ukumbi huo wakiwa na silaha za moto.
Kulingana na picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Mbunge Zaake alijaribu kurudisha kiti chake, ambacho mbunge Akol alikuwa amekikalia kwa muda na ndipo alipojaribu kumsukuma mbunge mwenzake kutoka kwenye kiti chake, jambo lililozua hisia kutoka kwa Akol, ambaye alisimama na kuanza kumshushia mangumi mfululizo na hatimaye kumwangusha Zaake chini.
Machafuko yaliendelea kuibuka huku Spika akiibua kanuni ya 9, na kutangaza “kukaa kwa uhuru” kutokana na idadi kubwa ya wabunge waliokuwepo kwenye vikao hivyo. Hali ya hewa ilibaki kuwa ya wasiwasi, na mzozo ukazuka, na kumlazimu Spika kuondoka kwa muda mfupi Bungeni.
Baada ya hayo, Spika alitangaza kuwasimamisha wabunge 12 Bungeni kwenye vikao vitatu mfululizo kutokana na kuhusika katika mtafaruku huo, akihusisha tabia zao na utovu wa nidhamu uliokithiri. Alisisitiza kuwa vitendo kama hivyo havikubaliki, akiangazia hitaji la adabu katika Bunge.