Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amekiri kuwa na furaha kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter Milan leo usiku nakutaja kutarajia mazuri kutoka kwenye klabu yake.
Arteta pia anasema yeye ni shabiki wa kocha wa Inter Simone Inzaghi na kazi yake. “Kweli, damu yangu inasukuma,” Mhispania huyo alianza.
“Tunakuja Milan kushinda na sio kushindwa.
Walicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa miaka miwili iliyopita – hizi ni aina ya michezo unayotaka kucheza.
“Nadhani Inter ina utambulisho wazi, na kocha anapaswa kusifiwa kwa hilo. “Anajua jinsi ya kupanga wachezaji katika njia zisizotarajiwa.
Ni changamoto ambayo pia tunapaswa kukabiliana nayo kwenye Ligi Kuu, na tutaona kesho jinsi ya kuishughulikia.”