Jeshi la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia watu 7 kwa tuhuma za wizi wa nyanya za shaba katika transifoma tano za shirika la Umeme Tanzania TANESCO katika mkoa huo na kusababisha hasara shirika hilo.
Taarifa hiyo imetolewa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Richard Abwao na amesema watuhumiwa hao wamebainika kuiba nyaya hizo huku wakitumia rasilimali za Tanesco kufanyia uhalifu huo.
“Jumla ya waya wa copper uliokamatwa ni armoured cable 6mmsq wenye kg 28.7, bare copper conductor 35 mmsq kg 9, na mfuko wa misumari ya inchi 2 kg 24.3 vyote vikiwa mali ya ya Tanesco” Richard Abwao
SACP Abwao amesema Jeshi hilo limeandaa operesheni maalumu ya kuwasaka watu wote wanojihusisha na biashara ya vyuma chakavu mitaani kwani wamegundua biashara hiyo inachochea wizi wa miundombinu ya serikali.
Kwa upande wake Mhandisi Amina Mohamed,Meneja wa Tanesco wa mkoa wa Tabora amesema wizi huo umesababisha hitlafu ya umeme ya mara kwa mara na kupelekea jamii kukosa huduma ya umeme.