Leo kumekuwa na mdahalo wa wgombea wa uongozi wa wafanyabiashara wa soko la kimataifa Karia koo ambao wagombea wanafasi ya kuanzia mwenyekiti mpaka mtumza fedha wa jumuiya ya wafanyabiashara hao walifika mbele ya wafanyabiashara kunadi hoja zao watakazoenda kutekeleza endapo wakipewa nafasi ya kuongoza katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi tarehe 20.
Itakumbukwa kwa mwaka huu ma mwaka jana wafanyabiashara wa soko la KKOO waligoma kwa kufunga maduka kwa siku kadhaa wakitaka baadhi ya kero zao hasa za kikodi ziwezwe kufanyiwa kazi ambapo serikali iliweza kuunda kamati maalum ya kuwasikiliza.