Mbunge wa jimbo la Kahama Jumanne Kishimba amehoji sababu za bodi ya mikopo nchini kutaka kuwafungulia mashtaka wahitimu wa vyuo vikuu wanaodaiwa marejesho ya mikopo wakati idadi kubwa hawajapata kazi.
Kishimba amehoji hilo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa mapendekezo ya mpango wa maendeleo ya Taifa na mapendekezo ya muongozo wa maandalizi ya mpango wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26 unaoendelea bungeni.
“Juzi bodi ya mikopo walileta hoja kwamba hawapati marejesho kwa watu waliokopa elimu na wanajiandaa kuanzac oparesheni ya kuanza kuwakamata wadaiwa wote hoja yangu ni Bodi ya mikopo alimpa mtu wa chuo hizo pesa mtu wa chuo akampa elimu mwanafunzi elimu ambayo haiajiriki sasa anayetakiwa kushtakiwa ni nani ni mwanafunzi au ni chuo kwasababu dunia inabadilika hatuwezi kuendelea na lugha ileile ya elimu ni ufunguo wa Maisha sasa hivi Elimu ni bidhaa wameshindwa kuuza kwahiyo mwenye kosa ni bodi ya mikopo” Jumanne Kishimba