Ripoti mpya imeeleza kuwa Wanajeshi wa Korea Kaskazini wanaopigana upande wa Urusi katika vita vya Ukraine wameanza kutazama maudhui ya ngono kwa kiasi kikubwa baada ya kuruhusiwa kutumia Mtandao kwa uhuru kwa mara ya kwanza.
Wanajeshi hao, ambao kawaida hawana ruhusa ya kuingia Mtandaoni bila vizuizi, sasa wamepata nafasi ya kujihusisha na maudhui haya baada ya Kim Jong Un kuwaruhusu kujiunga na juhudi za kijeshi za Urusi.
Kwa mujibu wa Gazeti la Financial Times, Mwandishi Gideon Rachman amesema Wanajeshi hawa 10,000 wamekuwa wakitumia nafasi hii mpya kwa ajili ya kutazama maudhui ya aina hii hali inayozua maswali kuhusu athari za kisaikolojia na kijamii kwa Wanajeshi ambao walikuwa wakibanwa dhidi ya maudhui kama haya na vizuizi vya kiutamaduni kutoka Korea Kaskazini.
Hata hivyo, Luteni Kanali Charlie Dietz wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani ameweka wazi kuwa hawezi kuthibitisha madai haya, akisisitiza kuwa Wizara inazingatia zaidi masuala muhimu ya kiusalama yanayohusiana na ushiriki wa Korea Kaskazini katika vita badala ya kuangalia maudhui wanayopata mtandaoni.