Jeshi la Nigeria limesema limewaua watu 481 na wengine zaidi ya 741 wanashikiliwa na jeshi hilo kufuatia operesheni ya kupambana na ugaidi iliyofanyika mwezi uliopita nchini humo.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Jeshi hilo Edward Buba alipozungumza na wanahabari mjini Abuja, na kuongeza kuwa, katika kipindi hicho, mateka 492 waliokolewa kutoka kwa watekaji wao katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo.
Pia amesema, katika kipindi hicho, jumla ya silaha 480 na risasi 9,026 zilikamatwa na jeshi hilo, na kuongeza kuwa, askari walifanikiwa kufichua maficho ya makundi yenye silaha katika maeneo mbalimbali nchini humo