Mashabiki wa mpira wa Israel wamekabiliwa na msururu wa mashambulizi katikati mwa Amsterdam, maafisa wanasema, huku polisi wa kutuliza ghasia wakilazimika kuingilia kati mara kadhaa kuwalinda.
Waziri Mkuu Dick Schoof alilaani “mashambulizi dhidi ya Wayahudi” na jeshi la Israeli lilizungumza juu ya “matukio makali na ya kikatili dhidi ya Waisraeli”.
Meya wa Amsterdam na mamlaka walisema kuwa licha ya kuwepo polisi wengi, mashabiki wa Israel wamejeruhiwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Uholanzi.
Wafuasi wa klabu ya Israel ya Maccabi Tel Aviv walikuwa wamesafiri hadi Amsterdam kwa mechi ya Ligi ya Europa dhidi ya Ajax.
Kabla ya mechi hiyo kulikuwa na fujo katikati mwa Amsterdam iliyohusisha mashabiki wa Maccabi na waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina, kukiwa na ripoti za wafuasi hao kufyatua fataki na kuangusha bendera ya Palestina.
Takriban watu 62 walikamatwa, polisi wa Uholanzi wanasema, na watu watano kupelekwa hospitalini