Rais wa Korea Kusini ameomba radhi kwa msururu wa mabishano yanayoendelea yanayomkabili mkewe ambayo ni pamoja na kudaiwa kukubali mkoba wa kifahari wa Dior na kujikusanyia mali isiyo halali.
Akihutubia taifa kwenye runinga, Yoon Suk Yeol alisema mke wake, Kim Keon Hee, alipaswa kujiendesha vyema zaidi, ulikuwa wa mbaya kupindukia, akiongeza kuwa baadhi ya madai dhidi yake “yalitiwa chumvi”.
Rais alisema ataunda ofisi ya kusimamia majukumu rasmi ya mke wa rais, lakini akakataa wito wa uchunguzi wa shughuli zake.
Msamaha wa Yoon ulikuja wakati anajaribu kubadilisha umaarufu wake kati ya umma wa Korea Kusini, unaohusishwa na utata unaozunguka mke wake
Chama cha upinzani pia kwa muda mrefu kimemshutumu mke wa rais kwa kuhusika katika udukuzi wa bei ya hisa na mapema mwaka huo, Yoon alipinga mswada wa kutaka mkewe achunguzwe kuhusu madai hayo pia