BARAFU YATANDA JANGWANI SAUDI ARABIA
Kitendo cha barafu kutanda jangwani ni nadra sana katika maeneo mbalimbali Duniani hasa katika maeneo ya jangwa anmbayo hujulikana kuwa na hali ya hewa ya ukame.
Sasa inaelezwa kuwa kwa mara ya kwanza barafu imeshuhudiwa ikiwa imetanda katika jangwa la Al-Jawf huko Saudia Arabia baada ya mvua kubwa kunyesha.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Saudia, tukio hilo lisilo la kawaida la hali ya hewa limesababisha maporomoko ya maji kwenye mito iliyokua imekauka na kujaza mabonde maji.
Baadhi ya Wananchi wa Saudia wameshiriki video na picha za tukio hilo katika mitandao ya kijamii na kuzua mijadala kila kona kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa Duniani.
Shirika la hali ya hewa la Saudi Arabia (NCM) limewaonya Raia wake kujiandaa kwa hali mbaya zaidi ya hewa katika siku zijazo baada ya mvua hiyo kubwa kunyesha wakitabiri kuwepo kwa vipindi vya upepo mkali na radi.