Wakili wa Mahakama Kuu Fernidand Makole amesema kwa mujibu wa sheria za Tanzania, taratibu za ukamataji zinamtaka Polisi akienda kumkamata Mtuhumiwa kwanza ajitambulishe na aonesha hati ya ukamataji (arrest warrant) akiwa na gari la Polisi linalotambulika ambapo amesema kwa aina ya tukio la kukamatwa kwa Mfanyabiashara Deogratius Tarimo eneo Kiluvya ni wazi ukamataji wake umekiuka sheria na waliohusika iwe ni Polisi au Watu wengine wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akiongea kwenye mahojiano maalum na @AyoTV, Makole amesema
“Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi ukiangalia hauoni kama Polisi wamekubali au wamekataa kwamba wanaoonekana mwenye video ambao ni ndio Watekaji au Wakamataji, kama ni Polisi au sio Polisi, kwa mujibu wa sheria inayozungumzia mwenendo wa makosa ya jinai taratibu za ukamataji zinamtaka Polisi akienda kumkamata Mtuhumiwa kwanza ajitambulishe, aonesha hati ya ukamataji (arrest warrant), sasa kwa aina ya video siwezi kucomment wale Watu walikuwa Polisi au sio Polisi kwakuwa taarifa ya Polisi haijasema lakini kama walikuwa Polisi aina ya ukamataji inakiuka sheria za Tanzania”