Mwanamke Mmoja anayefahamika kwa Jina la Sagali Masanja mwenye umri wa miaka 62,Mkazi wa kijiji cha Mahene wilayani nzega mkoani Tabora ameuawa kwa kukatwa katwa sehemu mbalimbali za mwili kisha wauaji hao kumkata titi moja na sehemu za siri na kuondoka nazo.
Akitoa taarifa ya tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi mwandamizi wa Jeshi hilo Richard Abwao amesema wauaji hao wa baada ya kukamilisha tukio hilo walikata sehemu baadhi ya mwili wa marehemu na kuondoka navyo huku cha ikiwa ni imani za kishirikina.
“Novemba 14,2024 katika kijiji cha Mahene,wilayani Nzega Mkoani Tabora majira ya saa saba na nusu Usiku kumetokea tukio la mauaji kwa mwanamke kukatwa katwa na panga kisha kuondoa sehemu za mwili kama titi na sehemu za siri kisha kuondoka na viungo hivyo.”Richard Abwao