Uongozi wa Yanga SC kupitia ukurasa wake wa instagram umetangaza rasmi kuwa umeachana na Kocha wao Mkuu Raia wa Argentina Angel Miguel Gamondi na Msaidizi wake Moussa Ndaw.
Taarifa hizo zinakuja ikiwa ni siku 8 zimepita toka Yanga SC impoteze michezo miwili mfululizo ya Ligi Kuu kwa kufungwa 1-0 na Azam FC na 3-1 na Tabora United.
Mengine yanayodaiwa kuchochea kufutwa kazi inadaiwa ni kutokuwa na maelewano mazuri na baadhi ya Wachezaji, Yanga hawajatangaza mbadala wake lakini yanahusishwa majina ya Mjerumani Sead Ramovic anayefundisha TS Galaxy ya Afrika Kusini, Kheireddine Madoui Raia wa Algeria aliyewahi kufundisha MC Oran na ES Setif na Moalin aliyekuwa KMC.