Mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 kati ya Paraguay na Argentina katika eneo la Amerika Kusini iligeuka kuwa aibu na wakukatisha tamaa kwa Lionel Messi.
Timu ya bingwa wa Kombe la Dunia ilipata kichapo cha 2-1, na mshambuliaji huyo alikosoa uchezaji wa waamuzi baada ya mechi.
Mwitikio huu unaweza kuwa umechangiwa na tabia ya mashabiki kwenye viwanja kwani wafuasi wa Paraguay mara kwa mara waliimba jina la “Ronaldo” wakati wa mchezo kama kejeli kwa Messi.
Baadhi ya mashabiki walihudhuria mechi hiyo wakiwa wamevalia jezi za timu ya taifa ya Ureno yenye jina la Cristiano Ronaldo mgongoni.
Jambo la kufurahisha ni kwamba hali hii ilianza Saudi Arabia, ambapo mashabiki waliohudhuria mechi za Cristiano Ronaldo walikuwa wakiimba jina la Messi kama uchochezi.