Katika kuendelea kuweka Mazingira rafiki ya ufanyaji Kazi kwa watendaji wa Kata Halmshauri ya Mji Ifakara Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro Mkurugenzi Mtendaji Halmashuri hiyo Bi. Zahara Michuzi ameacha kunununulia gari la kifahari lenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 186 badala yake fedha hizo amebadili matumizi kwa kufuata taratibu na kununua pikipiki 19 Kwa ajili ya watendaji hao.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo Michuzi amesema ameona ni busara kuendelea kutumia gari alilonalo.ili fedha hizo zitumike matumizi mengine kama vile kununua pikipiki hizo.
Amesema pikipiki hizo zimegharimu zaidi ya Shilingi million 60 ambapo amesema lengo kuendelea kutafuta njia mbalimbali za kuwafikia wananchi Ili kutatua changamoto zao Kwa haraka.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Danstan Kyobya amewataka watendaji kutumia pikipiki hizo katika matumizi yaliyokusudiwa
Kyobya amesema mpango wa kuwapatia pikipiki watendaji wa kata ni mzuri Kwani unaleta hamasa ya utendandaji kazi huku akimpongeza Mkurugenzi Michuzi Kwa kuacha kununua gari na fedha kuelekeza kununua pikipiki hizo
Nao baadhi ya watendaji hao wamemshukuru Mkurugenzi Michuzi Kwa kuwanajali na kwamba pikipiki hizo watazitumia vizuri lakini pia zitawasaidia kuwafikia wananchi Kwa haraka.
Wamesema awali walikuwa wakitumia gharama kubwa katika Usafiri lakini Kwa Sasa watakuwa na uwezo wa kufuatilia miradi ya maendeleo kwa ufanisi zaidi.