Zikiwa zimebaki siku chache kuelekea siku ya uchaguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu Wilaya ya Morogoro kupitia Viongozi wake imeendelea kuandaa matamasha ya kuhamasisha zoezi la wananchi kujitokeza kushiriki katika kupiga kura ampapo mara hii linafanyika hamasa ya mbio fupi
Mkuu wa Wilaya ya .Morogoro Mussa Kilakala ameongoza mbio hizo ambao amesema wamekuwa wakiandaa matamasha na hamasa mbalimbali ambazo zitawalenga vijana na wazee Ili makundi yote yaweze kujitokeza kupiga kura.
Anasema Kila mwananchi anitokeze siku hiyo bila wasiwasi kwani hali ya usalama Iko vizuri hakuna mtu atakaye weza kuharibu zoezi hilo.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro Emanuel Mkongo amesema kuwa zoezi la uandikishaji limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 100 na sasa kilichobaki ni wananchi kujitoa kwaajili ya kushiriki zoezi la upigaji kura na kumpata kiongozi atayewasaidia kwaajili ya maendeleo
Nao baadhi ya wadau walioshiriki katika zoezi hilo la mbio fupi wamesema kuwa wamejiandaa vyakutosha kuelekea uchaguzi huu huku wakiahidi kuwa mstari wa mbele kuchagua Viongozi
Uchaguzi wa Serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu Nchini kote na siku hiyo itakua siku ya mapumziko huku katika hamasa hiyo watu zaidi ya elfu Moja wajitokeza kushiriki.