Mainoo ameonyesha kwa klabu yake na nchi yake kwamba anaweza kuwa tegemeo katika timu ya Man U kwa miaka ijayo.
Kiungo huyo mchanga ameonyesha ukomavu zaidi ya umri wake na kuwasili kwa Amorim kunaweza kuwa bora kwake, pamoja na Yoro.
Meneja huyo wa Ureno anatarajiwa kuendelea kutumia mfumo wake wa 3-4-3 Old Trafford na Yoro anatarajiwa kuwa sehemu ya safu yake ya ulinzi ya wachezaji 3, pamoja na Lisandro Martinez na Matthijs de Ligt.
Beki huyo chipukizi hivi karibuni ataanza mechi yake ya kwanza ya kimashindano katika klabu hiyo baada ya kukaa nje kwa muda kutokana na jeraha alilolipata kwenye mechi za kujiandaa na msimu mpya.
Ujio wa Amorim umeleta matumaini kwa klabu na mafanikio yake akiwa na Sporting yamewapa mashabiki wa Man United matumaini ya mustakabali mwema.
Wakati huo huo, kuwasili kwa Amorim kunaweza kuwa mwanzo wa mwisho kwa Casemiro katika klabu hiyo.