Afisa wa Marekani anayesimamia mawasiliano ili kupata usitishaji vita kati ya Israel na Hezbollah inayoungwa mkono na Iran nchini Lebanon anatarajiwa kuzuru Beirut siku ya Jumanne, vyanzo vya habari nchini Lebanon vilisema Jumatatu, huku Beirut ikitarajiwa kutoa jibu lake kwa pendekezo la kusitisha mapigano la Marekani.
Diplomasia ya kusitisha mapigano inayoongozwa na Marekani imerejea tena kutiliwa maanani huku Israel ikizidisha mashambulizi yake: Mashambulio ya Israel katika vitongoji viwili vya Beirut yaliwauwa watu sita akiwemo afisa mmoja mkuu wa Hezbollah siku ya Jumapili, mara ya kwanza Israel kushambulia maeneo ya kati ya mji mkuu. katika mwezi mmoja
Pendekezo jipya la mapatano ya Marekani liliwasilishwa wiki iliyopita kwa Spika wa Bunge la Lebanon Nabih Berri, ambaye ameidhinishwa na Hezbollah kufanya mazungumzo.
Mjumbe wa White House Amos Hochstein alitarajiwa mjini Beirut siku ya Jumanne kwa mazungumzo juu ya usitishaji mapigano, chanzo cha kisiasa cha Lebanon kiliambia Reuters.
Mataifa yenye nguvu duniani yanasema usitishaji mapigano Lebanon lazima ujikite kwenye azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilimaliza vita vya mwaka 2006 kati ya Hezbollah na Israel.
Masharti yake yanaitaka Hezbollah kusogeza silaha na wapiganaji kaskazini mwa mto Litani, baadhi ya kilomita 20 kaskazini mwa mpaka.
Diplomasia imetatizwa na matakwa ya Israel ya kutaka uhuru wa kuchukua hatua iwapo Hezbollah itakiuka makubaliano yoyote, ambayo Lebanon imekataa