Kurejea kwa Mario Balotelli kwenye Serie A akiwa na Genoa kunakuja na mabadiliko hii ni baada ya mechi mbili pekee chini ya Alberto Gilardino, fowadi huyo anatazamiwa kufanya kazi na kocha mkuu mpya.
Kulingana na Matteo Moretto, usimamizi wa Genoa umeamua kuachana na Gilardino na nafasi yake itachukuliwa na Patrick Vieira, meneja wa zamani wa Nice, Strasbourg, na Crystal Palace.
Genoa kwa sasa inashika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Serie A baada ya raundi 12, pointi moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja.
Balotelli na Vieira hapo awali walifanya kazi pamoja huko Nice, ambapo uhusiano wao ulikuwa na mvutano.
Vieira, ambaye alicheza pamoja na Balotelli katika klabu ya Manchester City na Inter Milan, alimkosoa mshambuliaji huyo wakati walipokuwa Ufaransa, akidai kuwa mawazo ya Balotelli hayakufaa kwa michezo ya timu kama vile soka.
Jambo la kufurahisha ni kwamba Vieira pia alizingatiwa kwenye jukumu la usimamizi huko Rennes mapema mwaka huu kabla ya Genoa kupata huduma zake.