Ikulu ya Urusi imeonya kwamba uamuzi uliochukuliwa na Rais wa Marekani Joe Biden, wa kuiruhusu Ukraine kutumia makombora ya Marekani kushambulia ndani ya Urusi, unachochea mafuta kwenye moto, katika vita.

Urusi imesema uamuzi huo utazidisha mivutano ya kimataifa. Hii leo katibu wa masuala ya habari na mawasiliano Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov amekiambia kituo cha habari cha serikali TASS kwamba nchi hiyo tayari imefanya mabadiliko katika muongozo unaohusu silaha za Nyuklia na utaidhinishwa rasmi kama hatua muhimu.
kulingana na vyombo vya habari vya kimatsifs Peskov amesema, Rais Vladmir Putin ameshaweka wazi tangu mwezi Septemba, kwamba ikiwa Ukraine itatumia makombora hayo ya mataifa ya Kigeni kuishambulia ardhi yake, kutaiweka Jumuiya ya kijeshi ya NATO katika vita na Urusi.
Onyo la Urusi limetolewa wakati nchi hiyo ikiendelea kuishambulia Ukraine, huku ikiripotiwa kwamba watu wanane ikiwemo mtoto wameuwawa katika mkoa wa Sumy, kaskazini mwa Ukraine kufuatia shambulio la droni.