Wizara ya afya huko Gaza inayoendeshwa na Hamas ilisema Jumanne kwamba watu wasiopungua 43,972 wameuawa katika zaidi ya miezi 13 ya vita kati ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina.
Idadi hiyo inajumuisha vifo 50 katika muda wa saa 24 zilizopita, kwa mujibu wa wizara hiyo, ambayo ilisema watu 104,008 wamejeruhiwa katika Ukanda wa Gaza tangu vita vilipoanza wakati wapiganaji wa Hamas walipoishambulia Israel tarehe 7 Oktoba 2023.
Wapalestina watatu waliuawa siku ya Jumanne wakati wa operesheni ya kijeshi ya Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa karibu na Jenin, alisema gavana wa eneo hilo, akinukuu mamlaka za mitaa.
“Kuna miili mitatu ambayo sasa iko upande wa Israeli, baada ya kuwaua,” Kamal Abu al-Rub alisema, akinukuu Ofisi ya Uratibu ya Wilaya. Jeshi la Israel bado halijazungumza lolote kuhusu operesheni hiyo