Mdhamini na Mfadhili wa Yanga SC Ghalib Said Mohammed (GSM) leo amesherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa kwa namna ya kipekee Kongwa jijini Dodoma.
GSM amesherehekea kwa kutoa msaada wa madawati na pesa Tsh milioni 40 katika shule ya Msingi Mzogole pia ametoa msaada katika hospitali ya Kongwa wa Tsh milioni 60, seti ya kulelea watoto njiti pamoja na kuahidi kujenga njia za kuunganisha majengo ya hospitali hiyo.
Kwa upande wa Mke wa GSM Salha yeye amemjengea GSM Msikiti na kuutoa kama sadaka kwa ajili ya GSM kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.