Simba SC wamezindua jezi mpya za mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambazo watazitumia katika michezo yao yote ya Kimataifa ya msimu 2024/25.
Simba wamezindua jezi hizo za aina tatu za nyumbani, ugenini na jezi mbadala (third kit) na zimetengenezwa na mzalishaji wao wa siku zote Sandaland The Only One.